Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343 "KUHUSU KUKAA MITA 200" Inasema .......
MAZOEA YA KUWEPO UMBALI WA MITA 200 AU 300 KUTOKAKITUO CHA KUPIGIA KURA
Kumekuwepo na mazoea kwamba, baada ya kupiga kura wafuasiwa vyama hubakia na kukaa kwenye maeneo ya kupigia kuraumbali wa mita 100 au 200 au 300.Jambo hili ni kinyume na Sheria za Uchaguzi. Kwani, katikakifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343kinasema nanukuu
“Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura au;ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguziunaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita miambili yajingo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleoau nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”
Mwisho wa kunukuu.
Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali zaMitaa, Sura ya 292 kinasema, Nanukuu:
“hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigajikura katika uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa naumma ndani ya umbali wa mita mia tatu ya mlango wowote wakuingilia katika jengo, atavaa au kuonyesha kadi, upendeleo au 4nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”Mwisho wa kunukuu.
Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaelezamaana ya njia ya Umma.
Nanukuu:
“Public way includes any highway, market place, square, street,bridge or other way which is lawfully used by the public”
Mwisho wa kunukuu.
Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa aunafasi kwa wananchi kukusanyika bali zinapiga marufuku nakukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasasiku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.
Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio chakulinda kura.
Aidha, uzoefu unaonesha kwamba, katika kampenizinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa vyama tofautiwanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa nasehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafamajeruhi na uharibifu mali.
Source: http://www.nec.go.tz/uploads/documen...20UCHAGUZI.pdf
No comments:
Post a Comment