Friday, October 16, 2015

MAGUFULI ALIVYOITIKISA PEMBA


 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mikutano wa Gombani ya Kale, Pemba.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mke wa muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Abeid Aman Karume .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  akiteta jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli  katika mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi   katika uwanja wa Gombani ya kale Wilaya ya Chake chake Pemba
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein   akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM katika uwanja wa Gombani ya kale Wilaya ya Chake chake Pemba.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Pemba waliofurika kwenye uwanja wa mikutano wa Gombani ya Kale na kuwaambia wananchi hao kuwa umoja na mshikamano wetu utasaidia sana kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

 Maelfu ya wanaCCM waliofurika katika uwanja wa Gombani yakale Wilaya ya Chake chake Pemba wakimshangilia Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM kuomba Ridhaa ya kuchaguliwa katika nafasi ya kuiongoza Tanzania
 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment